Dries Van Agt, Waziri Mkuu wa zamani wa Uholanzi amesema Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netantahu ni mvunjaji mkubwa wa sheria za kimataifa. Katika barua yake kwa Uri Rosenthal, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi kuhusiana na safari inayotazamiwa karibuni hivi ya Benjamin Netanyahu nchini humo, Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Udachi amesema kuwa, Netanyahu amehusika mara kadhaa na ukiukaji wa sheria za kimataifa, hivyo, haoni faida yoyote kwa Waziri Mkuu huyo wa Israel kuruhusiwa nchi humo.
Van Agt ameashiria kuwa, Israel chini ya Netanyahu imekuwa ikikiuka mikataba iliyosaini yenyewe na kutoa mfano hai wa kipengee kimoja katika Mkataba wa Geneva, kinachosisitiza kulindwa kwa raia wakati wa vita na pia kingine katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya ukandamizaji. Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Uholanzi aidha ameita serikali ya nchi hiyo ilaani hatua ya Netanyahu kuendelea kuunga mkono ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa kizayuni katika ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu.
No comments:
Post a Comment