Maeneo ya Msimbazi
Waislamu jijini Dar es Salaam wameanza maandamano mchana huu kutokea katika misikiti mbalimbali iliyopo katika maeneo yao.
Askari wa jeshi la polisi wametanda kila kona ya jiji la Dar es Salaam ili kuzuia kufanyika kwa maandamano hayo, yenye kutaka kuachiwa huru kwa baadhi ya waislamu, akiwepo katibu wa jumuiya na taasisi za kiislamu nchini, Sheikh Issa Ponda wanaoshikiliwa na jeshi la polisi kwa makosa mbalimbali yakiwepo na uchochezi wa udini.
Katika maeneo ya kariakoo, hali imeanza kuwa tete kwani vurugu ni kubwa sana hivi sasa kati ya askari polisi na waislamu hao.
Kuna habari kuwa helikopta ya polisi zinarusha mabomu ya machozi kutoka angani sehemu za mskiti wa Mtambani, Kinondoni ili kutawanyisha waislamu wanaotaka kuandamana.
Mtaa wa Livingstone karibu na I&M Bank
Jijini Dar es Salaam hali si tofauti na hiyo maeneo ya Kariakoo maduka kadhaa yamefungwa kufuatia vurugu kama hizo baada ya Swala ya Ijumaa
Maeneo ya Posta karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani Askari wameweka utepe wa kudhibiti watu kuingia katika maeneo hayo kitendo kilichosababisha shughuli nyingi kusimama.
Mbagala
Msimabazi Kariakoo
Pichani ni Jeshi la Wananchi Tanzania maeneo ya Kariakoo kuongezea nguvu kwa ajili ya kutuliza ghasia. (Picha hii imepigwa na mdau Mpeli Jr Ngonywike kupitia mtandao wa facebook alipopiga picha hii kwa kujificha.
Kariakoo
Pande za Maktaba House
Vipeperushi vilivyotolewa na Waumini wa Dini ya Kiislamu kabla ya maandamano leo.
Polisi wakipita maeneo ya Mtambani-Kinondoni kuzuia maandamano ya leo
Kariakoo
ZANZIBAR
POLISI WAKITAWANYA WATU KWA MABOMU YA MACHOZI DARAJANI ZANZIBAR
Zanzibar Sakata la Waislamu kuendeleza kitimtim kufuatia kutoonekana kwa Kiongozi wa Kundi la Uamsho Vurugu zimeendelea kutawala eneo la Darajani na kusababisha Polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya watu.
Tutaendelea kutoa taarifa zaidi.