Jeshi la polisi limewafikisha katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu washtakiwa 11 akiwemo mfanyabishara Raza Hussein Ladha waliohusika na ujenzi wa jengo la ghorofa 16 lililoporomoka katika makutano ya mtaa wa indira gandhi na barabara ya Morogoro na kusomewa mashtaka 24 ya kuua bila ya kukusudia.
Source : ITV, ISSAMICHUZI
Mfanyabiashara Raza Hussein Ladha, Diwani katika Manispaa ya Kinondoni na wenzao 9 Jana walifikishwa Mahakamani wakikabiliwa na mashtaka 24 ya kuuwa bila ya kukusudia.
Mawakili wa utetezi waliiomba mahakama kutoa dhamana kwa wateja wao kwa sababu mashtaka ya kuua bila ya kukusudia yanayowakabili yanadhaminika.
Mawakili wa serikali walipinga maombi hayo wakisema kuwa wakati huu si wa kutoa dhamana kwa kuzingatia mazingira ya tukio lililosababisha kuwepo kwa kesi hiyo.
Kutokana na hoja hizo, Hakimu aliiahirisha kesi hiyo hadi April 16, mwaka huu atakapotoa uamuzi iwapo washtakiwa wapate dhamana au la.