Wapalestina wasiopungua wanne wameuawa shahidi baada ya ndege za utawala wa Kizayuni wa Israel usiku kushambulia maeneo kadhaa ya Ukanda wa Gaza. Ashraf al Qudwa Msemaji wa Wizara ya Afya ya serikali halali ya Palestina inayoongozwa na Hamas amesema kuwa, kombora la ndege ya Israel ilikita katika nyumba ya familia ya Abu Jalal, na kupelekea watu wanne wa familia hiyo kuuawa shahidi. Ameongeza kuwa, tokea yaanze mashambulizi ya kinyama ya Wazayuni huko Gaza siku ya Jumatano hadi sasa, zaidi ya watu 30 wameuawa shahidi na wengine 270 kujeruhiwa. Wakati huohuo, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel umekiri kuangushwa ndege ya kijeshi F16 katika anga ya Gaza. Brigedi ya Izzuddin Qassam tawi la kijeshi la HAMAS ilitangaza jana usiku kwamba ilitungua ndege ya kijeshi ya Israel katika eneo la magharibi mwa Ukanda huo. Kwa upande mwengine, William Hague Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uingereza ameitahadharisha Israel juu ya kuendeleza mashambulizi yake huko Gaza, na kusisitiza kuwa, bila shaka mashambulizi hayo yatakuwa na mwisho mbaya kwa utawala huo. Hague ameongeza kuwa, mashambulizi hayo yatapelekea Israel kukosa uungaji mkono wa jamii ya kimataifa. Hata hivyo, Hague ameshindwa kulaani jinai za majeshi ya Israel na badala yake amelaani mashambulizi ya roketi yaliyofanywa na wanamapambano wa Kipalestina dhidi ya vitongoji vya Israel.
Source: www.kiswahili.irib.ir
No comments:
Post a Comment