Free Palestine

Free Palestine

Saturday, November 17, 2012

AMIR WA QATAR ATUHUMIWA KUWAUZA HAMAS


Duru za kuaminika zinasema kuwa, safari iliyofanywa hivi karibuni na Sheikh Hamad bin Khalifa al Thani Amir wa Qatar katika eneo la Ukanda wa Gaza, ilifichua makazi ya viongozi kadhaa wa ngazi za juu Hamas. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la FARS NEWS, Sheikh Hamad bin Khalifa al-Thani aliwapa viongozi wote wa ngazi za juu wa Hamas zawadi za saa za mkononi na kalamu ambazo ndani yake mulikuwa na zana zilizokuwa zikiwasiliana na satalaiti za utawala wa Kizayuni wa Israel na kuwasaidia kuonyesha nyendo zao na mahala wanapoishi viongozi hao. Ahmad al Ja'abari mmoja kati ya makamanda wa ngazi za juu wa Izzuddin Qassam aliyeuawa shahidi siku chache zilizopita, alilengwa na ndege za kivita za Israel baada ya kufuatiliwa nyendo zake kwa usaidizi wa saa na kalamu alizopewa zawadi na Amir wa Qatar. Kwa upande mwengine, imeelezwa kuwa, Amir wa Qatar amemueleza wazi Ismail Haniya Waziri Mkuu wa serikali iliyochaguliwa na wananchi wa Palestina inayoongozwa na Hamas kwamba, kama wanataka misaada ya kifedha kutoka Qatar, wanapaswa kuacha kushirikiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wakati huhuo wautambue rasmi utawala wa Kizayuni wa Israel. Aidha Amir wa Qatar alitoa masharti matano kwa Harakati ya Hamas ili iweze kupata misaada ya kifedha na kiuchumi kutoka Qatar, ikiwa ni pamoja na kuacha kushirikiana na Iran, kuanzisha mazungumzo na utawala wa Kizayuni wa Israel bila ya masharti, kuutambua rasmi utawala wa Kizayuni wa Israel, kuitambua Quds Tukufu kuwa ni mji mkuu wa utawala huo ghasibu na kuacha kabisa muqawama na mapambano ya kutumia silaha.

No comments:

Post a Comment