Wanamapambano wa Palestina wametungua ndege ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel iliyokuwa inafanya mauaji dhidi ya wananchi wa Palestina.
Televisheni ya al Quds imezinukuu Brigedi za Izuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Palestina HAMAS zikisema kuwa, ndege za utawala wa Kizayuni zimefanya mashambulizi makali katika eneo ilipoanguka ndege hiyo ya Israel ili kufuta ushahidi na kuwazuia wanamapambano wa Palestina wasipate mabaki ya ndege hiyo.
Vile vile wanamapambano wa Palestina wamefanikiwa kwa mara ya kwanza kushambulia maeneo ya Wazayuni katika mji wa Baytul Muqaddas na kuzusha kiwewe katika safu za utawala wa Kizayuni.
Kabla ya hapo pia HAMAS ilikuwa imetungua ndege ya Israel isiyo na rubani na ilishambulia pia Tel Aviv mji mkuu wa utawala wa Kizayuni na kuwalazimisha viongozi wa Israel wakimbilie mafichoni.
Televisheni ya al Quds imetangaza pia kuwa wanapambanao wa Palestina wamelishambulia kwa kombora bunge la utawala wa Kizayuni, Knesset, huko magharibi mwa Baytul Muqaddas. Taarifa zinasema pia kuwa hoteli za kitalii za Wazayuni zimefungwa huko Baytul Muqaddas baada ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni ya mji huo kushambuliwa kwa makombora ya wanamapambano wa Palestina.
Source: www.kiswahili.irib.ir
No comments:
Post a Comment