Free Palestine

Free Palestine

Saturday, November 17, 2012

DRC YATAKA VIONGOZI WA RWANDA WAWEKEWE VIKWAZO


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameutaka Umoja wa Mataifa uweke vikwazo dhidi ya viongozi wa serikali ya Rwanda. Augustin Matata Ponyo amesema kuwa, Umoja wa Mataifa unapaswa kuweka vikwazo dhidi ya viongozi wa ngazi za juu wa Rwanda, kinyume cha hivyo taasisi hiyo ya kimataifa itapoteza itibari yake. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amelaani uungaji mkono wa Rwanda dhidi ya waasi wa M23 na kusisitiza kuwa, Umoja wa Mataifa unapaswa kuweka vikwazo dhidi ya Rwanda ikizingatiwa ripoti ya siri iliyotolewa na wataalamu wa umoja huo inayoelezea njama za viongozi wa Kigali za kuwapa silaha waasi hao. Kabla ya hapo, Umoja wa Mataifa ulizikosoa Rwanda na Uganda kwa kuwapa silaha na zana za kijeshi waasi wa M23 wanaopambana na serikali ya Kongo na kusababisha ukosefu wa amani katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo. Hata hivyo, nchi za Rwanda na Uganda mara kadhaa zimekadhibisha tuhuma hizo za wataalamu wa Umoja wa Mataifa za kuwapa silaha waasi wa M23.

No comments:

Post a Comment