Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa la Iran litajibu vikali hujuma na vitisho vyovyote dhidi yake.
Akizungumza Jumamosi katika mahojiano na Kanali ya Televisheni ya Mexico, Rais Ahmadinejad amesisitiza kuwa vikwazo vya nchi za Magharibi havijakuwa na athari katika mkondo wa ustawi wa taifa la Iran.
Kuhusu vitisho vya utawala wa Marekani dhidi ya Iran kutokana na shughuli zake za nyuklia zenye malengo ya amani, amsema kadhia ya nyuklia imebadilishwa kuwa ya kisiasa. Amesema ni wazi kuwa Marekani na waitifaki wake wanatumia kisingizio cha kadhia ya nyuklia ili kuzuia ustawi wa taifa la Iran. Rais wa Iran amesisitiza kuwa taifa lililostaarabika la Iran halihitajii bomu la atomiki na kuongeza kuwa wanaomiliki silaha za atomiki ni wale wasio na ustaarabu.
Rais Ahmadinejad amesema hadi sasa Iran ndio nchi iliyoshirikiana kwa karibu zaidi na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA. Kuhusu utawala wa Kizayuni wa Israel, Rais Ahmadinejad amesema Iran kamwe haitautambua utawala huo ghasibu kwani hata Umoja wa Mataifa umeshautangaza utawala wa Kizayuni kuwa ni mvamizi.
No comments:
Post a Comment