Thailand imekuwa taifa la kwanza kuitambua rasmi nchi huru ya Palestina mwaka huu wa 2012. Ujumbe wa Palestina katika Umoja wa Mataifa umesema umepokea barua kutoka kwa serikali ya Thailand inayosema kuwa, nchi hiyo ya kusini mashariki mwa bara Asia imeitambua rasmi nchi ya Palestina kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameipongeza Thailand kwa hatua hiyo aliyoitaja kuwa ya kutia moyo na yenye nafasi ya kipekee katika udiplomasia wa Palestina. Riyad al Maliki ameongeza kuwa, Thailand imekuwa nchi ya 131 kutambua rasmi nchi huru ya Palestina kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967.
Ni vizuri kuashiria hapa kuwa, Oktoba mwaka uliopita wa 2011, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO liliipatia Palestina uanachama kamili.
No comments:
Post a Comment