Viongozi wa Yemen wametangaza kuwa, Ali Abdallah Saleh dikteta wa nchi hiyo ameondoka katika uwanja wa ndege wa San'aa akielekea Marekani. Baadhi ya duru za Yemen zimetangaza kwamba, dikteta Ali Abdallah Saleh atakuwa nchini Oman kwa siku kadhaa kabla ya kuelekea Marekani.
Taarifa zaidi zinadai kwamba, dikteta huyo anakwenda Marekani kwa ajili ya matibabu na kwamba, atarejea Yemen baada ya kumaliza matibabu kwa ajili ya kukiongoza chama chake. Ali Abdallah Saleh aliondoka Yemen jana huku maandamano ya kupinga kupewa kinga ya kutoshtakiwa yeye na viongozi wenzake yakishadidi.
Maelefu ya wananchi wa Yemen waliandamana jana katika miji mbalimbali ya nchi hiyo wakitaka kunyongwa dikteta huyo. Wananchi hao walisikika wakipiga nara na kutoa wito wa kunyongwa Ali Abdallah Saleh waliyemtaja kuwa mchinjaji na muuaji.
No comments:
Post a Comment