Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limeikosoa Marekani kutokana na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu inaoufanya.
Taarifa ya Human Rights Watch imeashiria kuweko wafungwa milioni mbili na laki tatu katika jela za Marekani na kuikosoa nchi hiyo kutokana na kuwa na wafungwa wengi zaidi duniani. Shirika la Kutetea Haki za Binadamu limekosoa sheria kali za Marekani kwa wahajiri ambazo limesema zimekuwa chanzo cha mamia kwa maelfu ya watu kutupwa jela.
Mfumo wa kimahakama wa Marekanin pia umekosolewa mno na ripoti ya Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch huku taarifa hiyo ikiwaonya viongozi wa Washington kuhusiana na kuendelea kuwashikilia watuhumiwa wa vitendo vya ugaidi katika jela ya Guantanamo.
No comments:
Post a Comment