Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov
Umoja wa Ulaya EU mapema leo umepitisha vikwazo vipya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Vikwazo hivyo vimelenga Benki Kuu ya Iran pamoja na sekta ya mafuta. Hata hivyo Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov amesema vikwazo hivyo ni vya upande mmoja na visivyofaa.
Lavrov amekumbusha kuwa vikwazo hivyo vitawaathiri zaidi wanachama wa EU hususan nchi kama Ugiriki, Italia na Uhispania ambazo zinaagiza kwa wingi mafuta kutoka Iran. EU imesema vikwazo vya mafuta vitaanza kufanya kazi kuanzia Julai 1 mwaka huu. Russia imesema hilo linaonyesha wasiwasi wa umoja huo kuhusiana na uamuzi wao huo usio wa busara.
Punde baada ya EU kutangaza vikwazo hivyo nchi mbalimbali za Afrika na Asia zimetuma maombi kwa Iran zikitaka kuruhusiwa kuagiza mafuta kutoka hapa nchini.
No comments:
Post a Comment