Free Palestine

Free Palestine

Monday, January 23, 2012

Gazeti la Marekani laitaka Mossad kumuua Obama


Gazeti moja la Mayahudi wa Marekani limeliomba Shirika la Ujasusi la Israel Mossad kumuua Barack Obama likidai kuwa, Rais huyo wa Marekani amekuwa na mielekeo ya kiadui kwa Israel. Gazeti hilo liitwalo Atlanta Jewish Times limeandika kuwa, kuendelea kuwa uongozini Rais Obama kunahatarisha mustakabali wa utawala huo haramu. 

Katika makala ya hivi karibuni iliyoandikwa na Andrew Adler, mwasisi wa gazeti hilo la Kiyahudi la Marekani, amemtaka Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aiamrishe Mossad kumuua Obama ili kuhifadhi na kulinda uwepo wa utawala huo wa kizayuni.

No comments:

Post a Comment