Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO amesema kuwa ukosefu wa uadilifu wa kijamii katika nchi tajiri ulimwenguni unazidi kuongezeka.
Bi Margaret Chan, raia wa China, alisema hayo jana katika kikao cha WHO kilichofanyika mjini Geneva Uswisi na kuongeza kuwa, ukosefu huo wa uadilifu katika baadhi ya nchi tajiri duniani unashuhudiwa zaidi katika hali ya maisha baina ya watu wazee na vijana.
Dk. Chan ameongeza kuwa, ukosefu wa uadilifu katika kipato cha watu wa nchi hizo tajiri ni mkubwa mno kiasi kwamba haujawahi kushuhudiwa mfano wake katika kipindi cha miaka 25 iliyopita.
Ukosefu wa uadilifu unaongezeka pia baina ya nchi na nchi na baina ya mataifa tajiri na mataifa maskini duniani, huku mataifa ya kibepari yakizidi kuzinyonya nchi changa ulimwenguni.
Dk. Margaret Chan amesema pia kuwa idadi ya vifo vya watoto wadogo iliongezeka sana mwaka 2011 idadi ambayo haijawahi kushuhudiwa mfano wake katika kipindi cha miaka 60 iliyopita.
No comments:
Post a Comment