Jumuiya ya Nchi Zisizofungama na Siasa za Upande Wowote NAM imelaani ukiukaji wa anga ya Iran uliofanywa na ndege ya ujasusi ya Marekani isiyo na rubani mwishoni mwa mwaka jana. Kitengo cha mawasiliano cha jumuiya ya NAM kimetoa taarifa kikilaani ukiukaji huo uliofanywa na ndege ya ujasusi ya Marekani isiyo na rubani katika anga ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM ambayo ina wanachama 120 imeeleza katika taarifa yake kuwa, ukiuaji wa anga ya Iran ni kinyume na sheria zote za kimataifa zinazohusiana na mamlaka ya kujitawala ya anga za nchi mbalimbali. Mapema mwezi huu Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC pia ilikemea hatua hiyo ya ndege ya ujasusi ya Marekani ya kuingia katika anga ya Iran kinyume cha sheria. Disemba 4 mwaka jana Iran ilitangaza kuwa kitengo chake cha masuala ya kielektoroniki katika vikosi vya jeshi kimefanikiwa kuidhibiti ndege hiyo ya ujasusi ya Marekani aina ya RQ-170 Sentinel ambayo ilikuwa ikipaa katika anga ya mji wa Kashmar huko kaskazini magharibi mwa Iran na baadae kuishusha chini.
No comments:
Post a Comment