Free Palestine

Free Palestine

Friday, March 09, 2012

KENYA YAWATAKA WAUGUZI WASIO NA KAZI KUPELEKA MAOMBI YAO ILI KUJAZA NAFASI ZA WAUGUZI WALIOFUKUZWA


Waziri wa Huduma za Afya wa Kenya amesema kuwa, Serikali ya nchi hiyo wiki hii itawataka watu wote waliomaliza masomo ya uuguzi na ambao hawajaajiriwa na wale wote waliostaafu watume maombi yao kwa wizara hiyo ili waweze kuziba pengo la wafanyakazi 30,000 wa huduma za afya ambao wamegoma kufanya kazi tangu Alkhamisi iliyopita. 

Waziri Bw. Anyang' Nyong'o amesema hayo huku kukiwa na habari kuwa serikali ya Kenya imewafuta kazi wafanyakazi wa huduma za afya waliogoma nchini humo wakitaka nyongeza ya mishahara na mazingira mazuri ya kufanyia kazi.
 
Hii ni katika hali ambayo jana msemaji wa serikali ya Kenya Alfred Mutua alitangaza kuwa, wafanyakazi 25 elfu wa vituo vya afya wamefukuzwa kutokana na kushiriki katika mgomo. 
Mutua amesema, tayari majina ya walioshiriki kwenye mgomo humo yameondolewa katika orodha ya waajiriwa wa Serikali. Amefafanua kuwa, serikali ya nchi hiyo haiwezi kuendelea kuvumilia kuwaona wagonjwa wakiteseka bila sababu kutokana na mgomo.

No comments:

Post a Comment