Free Palestine

Free Palestine

Friday, February 24, 2012

WIZI WATOKEA KATIKA BUREAU DE CHANGE MOJA MAARUFU MJINI DAR ES SALAAM ASUBUHI LEO

Kuna wizi umetokea katika Bureau de chnage maarufu hapo mjini inayojulikana kama SAHARA BUREAU DE CHANGE katika majira ya saa nne asubuhi leo tarehe 24.02.2012

Nilipofika Sehemu ya tukio nilikuta Maaskari wameshafika na wameshaanza zoezi la upelelezi.

Kwa Taarifa nilizozipata kutoka kwa bureau operator nilipoongea naye alisema wezi hao wawili waliingia kama wateja wa kawaida.

Mara baada ya kuingia walitoa bunduki lao ndogo na spray ya kuwalaza hao. Wateja wengine waliokuwa ndani walilazwa chini, Operator aliambiwa na wezi hao waonyeshwe Safe ya hela..

Walipoonyeshwa safe ya hela operator na msaidizi wake na wateja wengine wote walipuliziwa ile spray ili wasinzie..

Hapo ndipo wezi wakabeba Hela Zote ndani ya Bureau Hiyo na kutoka kimya kimya bila ya mlinzi wa nje ya bureau hiyo kujua kilichotokea huko ndani.

Mpaka nilipoondoka niliwaacha maaskari wakifanya maswali na mjibu na watu wa bureau hiyo.

No comments:

Post a Comment