Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, serikali za nchi za Ulaya zinapaswa kujilaumu zenyewe kutokana na matatizo ziliyowasababishia wananchi wao.
Bw. Ramin Mehmanparast ameongeza kuwa, wananchi wa Ulaya wanapaswa kujua kuwa matatizo yote yanayowakabili yanatokana na siasa mbovu za watawala wao.
Pia amesema, kutokana na mitazamo yake ya kibinaadamu, Iran haipendi kuona wananchi wa Ulaya wanateseka katika kipindi hiki cha baridi kali na mgogoro mkubwa wa kiuchumi, lakini pamoja na hayo imelazimika kuchukua hatua kali za kukata kuziuzia mafuta baadhi ya nchi za Ulaya na kutishia kuacha kuziuzia mafuta yake nchi nyingine zote za bara hilo kutokana na siasa za kiadui za viongozi wa Ulaya dhidi ya Iran.
Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza katika mahojiano aliyofanyiwa na kanali ya 3 ya televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwamba, Tehran inajua kuwa nchi za Ulaya hivi sasa zinahitajia sana nishati kutokana na msimu wa baridi kali na mgogoro mkubwa wa kiuchumi, lakini watawala wa nchi za Ulaya nao inabidi wajue kwamba, wanapaswa kuwa na siasa sahihi mbele ya mataifa mengine ili wasiwasababishie matatizo kama ya hivi sasa wananchi wao.
No comments:
Post a Comment