Free Palestine

Free Palestine

Wednesday, February 22, 2012

Askari wa Marekani wachoma moto Qur'ani Tukufu


Wananchi wa Afghanistan wamefanya maandamano makubwa ya kulaani kitendo cha vikosi vya majeshi ya Marekani kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu. 
Wananchi hao wameandamana katika barabara za mji wa Kabul na nje ya kambi ya jeshi la anga la Marekani ya Bagram. Waandamanaji hao waliokuwa wamejawa na ghadhabu kwa kitendo hicho walichokiita cha kijuba cha askari wa Marekani, wamesikika wakipiga nara za mauti kwa dola hilo la kibeberu na kutoa wito wa wahusika wa uhalifu huo kufikishwa mbele ya sheria. 
Aidha, maandamano ya kulaani kitendo hicho cha kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu, yameripotiwa katika miji mingine ya Afghanistan.
Ni vizuri kuashiria hapa kuwa, Aprili mwaka jana 2011, watu zaidi ya 10 waliuawa katika maandamano ya siku kadhaa nchini Afghanistan, baada ya Kasisi Terry Jones wa Marekani kuteketeza kwa moto nuskha za Qurani Tukufu katika jimbo la Florida.

No comments:

Post a Comment