Free Palestine

Free Palestine

Saturday, January 21, 2012

SARKOZY AKIRI KUWA VITA DHIDI YA IRAN VITAKUWA NA HASARA KUBWA


Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa ametahadharisha kwamba kuvamiwa kijeshi Iran kwa sababu ya miradi yake ya nyuklia kutaibua maafa makubwa duniani ikiwa ni pamoja vita na machafuko katika eneo zima la Mashariki ya Kati. 
Sarkozy amekiri hayo na kuongeza kwamba Paris itafanya kila iwezalo ili kujiepusha kushiriki katika vita dhidi ya Iran. 
Inafaa kukumbusha hapa kuwa Marekani na Israel mara kadhaa zimetishia kuishambulia kijeshi Iran kwa madai yasiyo na msingi kwamba miradi ya nyuklia ya Tehran eti lengo lake ni kutengeneza silaha za nyuklia. 
Hii ni katika hali ambayo Iran mara kadhaa imekanusha madai hayo na kutangaza kwamba miradi yake ya nyuklia ni ya kiraia na inaendeshwa kwa mujibu wa Maktaba wa N.P.T, chini ya usimamizi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki.

No comments:

Post a Comment