Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran amesema leo kuwa, vikwazo vya upande mmoja vya Umoja wa Ulaya (EU) dhidi ya Iran vinalenga kuchachawiza uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kufanyika mwezi Machi mwaka huu lakini hilo halitawezekana. Ayatullah Ahmad Khatami amesema vikazo hivyo vya EU ambavyo lengo lake lingine ni kulemaza uchumi wa Iran, vitaambulia patupu kwa uchumi wa taifa hili umejengeka juu ya misingi thabiti na imara. Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa Tehran amesisitiza kuwa miamala kama hiyo ya kijuba haitakuwa na natija yoyote kwa Wamagharibi ghairi ya kulemaza chumi zao wenyewe.
No comments:
Post a Comment